Zabihullah Mujahid ameyasema hayo akikanusha na kutaja kuwa ni uvumi usio na msingi taarifa inayodai kwamba ndege moja ya kijeshi ya Marekani imeingia kwenye kituo cha anga cha Bagram na kusisitiza kwa kusema: "haiwezekani wanajeshi wa Marekani kuja Afghanistan".
Zabihullah Mujahid ameeleza kuwa Afghanistan ni nchi huru na akaongeza kuwa, Serikali ya muda ya Afghanistan haitaruhusu kitu kama hicho kwa nchi yoyote ile.Msimamo huo umetangazwa huku baadhi ya vyombo vya habari na kurasa za mitandao ya kijamii zikidai kuwa naibu mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) aliingia kwa siri katika Kituo cha Anga cha Bagram kwa kutumia ndege ya kijeshi.
Aidha, imedaiwa katika siku za hivi karibuni kwamba Taliban imekikabidhi kituo cha kijeshi cha Bagram kwa Marekani.Taarifa hizo zinatolewa katika hali ambayo tangu Rais wa Marekani Donald Trump alipoingia tena Ikulu ya White House amekosoa mara kadhaa hatua ya nchi hiyo ya kuutelekeza uwanja wa ndege wa Bagram na kudai kwamba, baada ya Marekani kuondoka Afghanistan, uwanja huo wa ndege umekabidhiwa kwa China.
Na hii ni katika hali ambayo, kabla ya hapo ulienezwa pia uvumi wa China kukabidhiwa kituo cha anga cha Bagram, dai ambalo maafisa wa serikali ya muda ya Afghanistan walilikanusha pia.Katika siku za hivi karibuni, ujumbe wa Marekani uliojumuisha mjumbe wa zamani wa nchi hiyo katika masuala ya Afghanistan, Zalmay Khalilzad, ulisafiri kuelekea Kabul kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka minne na kukutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya maafisa wa serikali ya muda ya nchi hiyo.../
342/
Your Comment